Bonyeza hapa upate orodha ya masomo.
Toleo la kwanza. Somo hili linaweza kuboreshwa kadiri muda unavyoendelea.
Somo la 2 — Matendo 2: Moto na Maandiko: Pentekoste na Mahubiri ya Kwanza
WAZO KUBWA
Moto wa Roho ulioshuka Pentekoste haukupita pembeni ya Maandiko; uliwasha Maandiko kama moto. Roho Mtakatifu alipokuja, kanisa halikuhubiri Roho — walihubiri Yesu, kutoka Agano la Kale. Moto na Maandiko vinakutana, na roho elfu tatu zinaongezwa siku moja. Roho anazaa kanisa si katika mystique iliyotengwa, lakini kwa njia ya Neno la Kristo linalotangazwa.
SEHEMU YA 1 — USOMAJI WA MAANDIKO: MATENDO 2:1–47
Kabla hujasoma kitu kingine katika somo hili, fungua Biblia yako Matendo 2 na usome sura yote polepole, kwa sala, mpaka mwisho. Ukiweza, isome mara mbili — mara moja ili kusikia rythme, mara ya pili ili kutia alama kile kinachokugusa. Pigia mustari kile kinachoamsha moyo wako.
Matendo 2 inajigawanya kwa kawaida katika mouvements ine: kuja kwa Roho (mistari 1–13), mahubiri ya Petro (mistari 14–36), jibu la watu na mwito wa kutubu (mistari 37–41), na picha ya kanisa la kwanza lililokusanyika kuzunguka Neno, ushirika, mkate, na sala (mistari 42–47). Zote ine zinashikamana. Pentekoste si upepo na moto tu; ni upepo na moto vinavyozaa Kristo anayehubiriwa na communauté inayoabudu.
MSTARI WA MSINGI — MATENDO 2:42
“Walidumu katika mafundisho ya mitume, na katika ushirika, na katika kumega mkate, na katika sala.”
SEHEMU YA 2 — KUTEMBEA KATIKA MATENDO 2
A. Pentekoste — Siku Iliyokuwa Tayari Kwenye Calendrier ya Mungu
Matendo 2 inapofunguka, Luka anaandika kwamba “siku ya Pentekoste ilipofika.” Namna hiyo ya kusema ina maana. Pentekoste haikuwa sikukuu mpya iliyobuniwa na kanisa. Ilikuwa Sikukuu ya Majuma (Shavuot), moja kati ya sikukuu tatu kubwa za hija za Israeli, iliyosherehekewa siku makumi tano baada ya Pasaka. Ilikuwa sikukuu ya mavuno — malimbuko ya mavuno ya ngano. Na katika mapokeo ya Wayahudi ya baadaye, ilihusishwa na kutolewa kwa Sheria pale Sinai.
Timing hiyo haikuwa hasard. Yesu hakumimina Roho tu wakati aliouchagua peke yake. Alimimina Roho siku iliyokuwa tayari imetiwa alama, tayari takatifu, tayari ikielekeza mbele. Mungu alikuwa akiandaa wakati huu kwa karne nyingi. Mungu yule yule aliyeweka calendrier ya Israeli ndiye aliweka calendrier ya kanisa.
Kila wakati Agano Jipya linatimiza Agano la Kale, mambo mawili ni kweli kwa wakati mmoja: linatushangaza, na halitushangazi. Linatushangaza kwa sababu hatukuliona likija. Halitushangazi kwa sababu, tunapoangalia nyuma, tunaona kwamba Mungu alikuwa anazungumza juu yake wakati wote.
Pentekoste inatukumbusha kwamba Roho na Baba wanafanya kazi kama mmoja. Ahadi inatoka kwa Baba (Matendo 1:4); zawadi ni Roho; siku ilikuwa imewekwa zamani.
B. Upepo, Moto, Lugha — Pentekoste Ilionekana Namna Gani
Ghafla sauti ikatoka mbinguni, kama upepo mukali unaovuma. Ndimi zilizoonekana kama moto zikatokea na kukaa juu ya kila mmoja. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha nyingine.
Ona mambo tatu kwa makini sana.
Kwanza, ilikuwa sauti kutoka mbinguni. Initiative ilikuwa ya Mungu. Hawakupanda juu kwenda kuchukua Roho. Yeye alishuka kwao. Hivyo ndivyo Roho anavyotenda kila mara. Tunajiandaa. Tunasali. Tunangoja. Lakini Roho anatolewa; hachukuliwi kwa nguvu.
Pili, moto ulikaa juu ya kila mmoja. Huu ndio ukuhani wa kila muamini. Moto haukukaa juu ya Petro peke yake, juu ya mitume peke yao, juu ya wanaume peke yao, au juu ya viongozi peke yao. Ulikalia kila mmoja — wanaume na wanawake, vijana na wazee, wanaojulikana na wasiojulikana. Roho hana upendeleo. Anajaza.
Tatu, walisema kwa lugha nyingine — na neno ambalo Luka anatumia ni glōssais, neno lile lile linalotumiwa kwa “ndimi.” Hizi zilikuwa lugha zinazojulikana za mataifa yaliyokusanyika Yerusalemu. Karama ya kwanza ya muujiza ya Roho haikuwa experience ya privé kwa chumba cha juu. Ilikuwa zawadi iliyolengwa nje, kwa mataifa.
C. Lugha za Mataifa — Babeli Iliyokombolewa
Soma polepole liste ya mataifa katika Matendo 2:9–11: Waparthi, Wamedi, Waelami, wakaaji wa Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na sehemu za Libya karibu na Kirene, wageni kutoka Roma, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu. Luka anachora picha. Dunia yote iliyojulikana iko Yerusalemu, na wote wanasikia matendo makuu ya Mungu kwa lugha zao wenyewe.
Katika Mwanzo 11, kwenye Mnara wa Babeli, kiburi cha wanadamu kilijenga mnara kufika mbinguni. Mungu alisambaza mataifa na kuchanganya lugha zao. Tangu siku hiyo, familia ya wanadamu iligawanyika.
Katika Matendo 2, Roho anashuka. Hafuti lugha — anazijaza. Harudishi mataifa kwenye lugha moja. Anatangaza matendo ya Mungu kwa kila lugha. Pentekoste si Babeli kufutwa; ni Babeli kukombolewa. Ukuta wa kutenganisha unaanza kuanguka, si kwa wote kuwa sawa, bali kwa injili kufikia kila ulimi.
Hili lina maana kwa missions zetu katika Afrika, Canada, Ulaya, na kila mahali. Injili si message ya Magharibi iliyovikwa lugha ya Magharibi. Roho wa Pentekoste anazungumza Kinyarwanda, Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Lingala, Luganda, Kiarabu, na kila lugha ya kila watu. Lugha yako si ndogo sana kwa Roho. Culture yako si ndogo sana kwa injili.
D. Zarau na Kutoelewa — “Wamelewa Mvinyo Mpya Sana”
Luka anaandika kwamba wengine katika umati walishangaa na kuchanganyikiwa, lakini wengine walidhihaki: “Wamelewa mvinyo mpya sana.” Hata Pentekoste, pamoja na uwepo wa Mungu ulioonekana wazi, kulikuwa na kutokuamini.
Tia hili maanani, kwa sababu litarudi tena katika Kitabu cha Matendo. Kila mahali Roho anapotembea, majibu mawili yanatokea: imani na zarau. Njaa na uadui. Tusishangae ushuhuda wetu unapokataliwa. Tusivunjike moyo wakati wengine wanacheka mambo ya Mungu. Kazi ya Roho imekutana kila mara na majibu yote mawili.
Kilicho muhimu ni kile mitume walifanya na zarau hiyo. Hawakurudi nyuma. Hawakubishana. Petro alisimama, akainua sauti yake, na akahubiri.
E. Petro Anasimama Pamoja na Wale Kumi na Moja — Kuhubiri Katika Communauté
Matendo 2:14 inasema “Petro akasimama pamoja na wale kumi na moja, akainua sauti yake.” Ona détail ndogo: pamoja na wale kumi na moja. Petro si mhubiri solo. Wale Kumi na Wawili wako karibu naye. Kanisa linahubiri kama mwili.
Hili lina maana kwetu. Hatusimami peke yetu katika huduma. Mimbari inabebwa na wazee, waombezi, na watumishi waliojificha. Unaposhuhudia nyumbani au kazini, mwili wa Kristo unasali kwa ajili yako. Husemi peke yako kamwe. Wale kumi na moja wanasimama na yule mmoja — na Kristo anasimama nao wote.
Hii pia ndiyo sababu Petro, ambaye wiki chache mbele alikana Bwana mara tatu karibu na moto, sasa anaweza kumuhubiri Bwana bila woga. Roho alikuwa amemurudisha. Communauté ilikuwa imemupokea tena. Kushindwa hakukufanyi usitumike na Mungu; kinachokufanya usitumike ni kukataa kutubu. Kama umejikwaa, inuka. Roho yuko katika kazi ya kurudisha wavuvi na kuwafanya wahubiri.
F. Ahadi ya Yoeli — Siku za Mwisho Zimeanza
Hatua ya kwanza ya Petro si kueleza experience. Hatua yake ya kwanza ni kufungua Biblia. Anaenda kwa Yoeli 2:28–32: “Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya watu wote...”
Mambo tatu katika nukuu ya Petro yanahitaji attention yetu.
Kwanza, “katika siku za mwisho.” Petro anatangaza kwamba siku za mwisho zimeanza. Si baadaye. Si katika future ya mbali tu. Siku za mwisho zilianza Roho alipomiminwa Pentekoste. Tumekuwa tukiishi katika siku za mwisho kwa miaka elfu mbili. Kila génération ya kanisa ni génération ya siku za mwisho, inayoitwa kuwa tayari, inayoitwa kuwa mashahidi.
Pili, “juu ya watu wote.” Juu ya wana na binti. Juu ya vijana na wazee. Juu ya watumishi. Roho anafanya unabii usiwe mali ya groupe ndogo. Hatolewi tu kwa classe ya kidini. Anamiminwa juu ya mwili wote.
Tatu, “kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.” Hapo tena — Jina. Kama tulivyosema katika Somo la Kwanza kwamba rythme ya Matendo ni kujua Neno, kutumainia Roho, na kuhubiri Jina, tunaona tayari katika Matendo 2 kwamba Yoeli mwenyewe alikuwa anaelekeza kwenye Jina. Kuja kwa Roho kulikuwa kila mara kuongoza watu kuliitia Jina la Bwana. Pentekoste ni kwa ajili ya proclamation.
G. Moyo wa Mahubiri — Kristo Amefufuka na Ametawazwa
Sasa Petro anafanya kile kila mhubiri aliyejaa Roho lazima afanye: anahubiri Kristo. Hahubiri juu ya Roho Mtakatifu. Anahubiri Yesu, na anamuhubiri kutoka Agano la Kale.
Anaenda kwa Zaburi 16: “Hutaacha nafsi yangu Kuzimu, wala hutamwacha Mtakatifu wako aone uharibifu.” Anaweka hoja: Daudi alisema haya, lakini Daudi alikufa na akazikwa, na kaburi lake liko hapa Yerusalemu. Basi Daudi alikuwa anazungumza juu ya nani kweli? Alikuwa anatabiri ufufuo wa Masihi.
Kisha Petro anaenda kwa Zaburi 110:1: “Bwana alimwambia Bwana wangu, keti mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye adui zako kuwa kiti cha miguu yako.” Tena — Daudi hangeweza kuwa anazungumza juu yake mwenyewe tu. Daudi alikuwa anazungumza juu ya Masihi, ambaye sasa ametukuzwa mkono wa kuume wa Baba.
Hitimisho linashangaza: “Basi nyumba yote ya Israeli ijue kwa hakika kwamba Mungu amemufanya kuwa Bwana na Masihi, Yesu huyu muliyemusulubisha.”
Huu ndio moyo wa mahubiri ya kwanza ya Kikristo, na ndio moyo wa kila mahubiri ya Kikristo yaliyowahi kuwa ya uaminifu: Yesu yuko hai. Yesu ametawazwa. Yesu ni Bwana. Yesu ni Masihi. Agano la Kale lilikuwa likielekeza kwake kila wakati.
Ona kwa makini: Petro hahubiri karama za Roho. Anahubiri ufufuo na ubwana wa Kristo. Kazi ya Roho si kujitukuza yeye mwenyewe; kazi ya Roho ni kumutukuza Kristo (Yohana 16:14).
H. “Tufanye Nini?” — Kuchomwa Moyoni
Matendo 2:37 inasema, “Waliposikia haya, wakachomwa mioyoni mwao, wakamwambia Petro na mitume wengine, ‘Ndugu, tufanye nini?’”
Hivi ndivyo mahubiri ya kweli hufanya. Yanakata. Yanachoma. Hayabembelezi kiburi; yanashawishi na kuhukumu moyo. Roho, akifanya kazi kupitia Neno, anafunua moyo na analeta swali kwenye midomo: Tufanye nini?
Jibu la Petro liko wazi: “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa Jina la Yesu Kristo kwa msamaha wa zambi zenu, nanyi mutapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.” Hapo iko pattern ya injili: tubu, amini, batizwa, pokea.
Kisha anapanua mulango: “Ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali — wote ambao Bwana Mungu wetu atawaita.” Kwa wote walio mbali. Hao ni sisi. Hilo ni kanisa la Afrika. Hilo ni kanisa la Canada. Hilo ni kila taifa, kila kabila, kila ulimi. Ahadi inafika mbali kadiri mwito unavyofika.
I. Elfu Tatu Wanaokoka — Echo ya Sinai Iliyogeuzwa
Matendo 2:41 — “Wale waliolipokea neno lake wakabatizwa, na siku ile wakaongezeka karibu watu elfu tatu.”
Namba hii si hasard. Wakati Musa alishuka kutoka Sinai na Sheria, siku makumi tano baada ya Pasaka, watu elfu tatu walihukumiwa kwa kuabudu ndama wa zahabu (Kutoka 32:28). Pentekoste, siku makumi tano baada ya Mwana-Kondoo wa Pasaka wa Mungu kuchinjwa na kufufuka, watu elfu tatu wanaokoka.
Tarehe ile ile. Namba ile ile. Matokeo mawili yaliyo kinyume. Sinai, herufi iliua elfu tatu. Pentekoste, Roho alitoa uzima kwa elfu tatu. “Herufi huua, lakini Roho huhuisha” (2 Wakorinto 3:6). Hii si coincidence ya ujanja. Ni injili iliyoandikwa ndani ya calendrier ya Mungu.
J. Pattern ya Kanisa la Kwanza — Neno, Ushirika, Mkate, Sala
Matendo 2:42–47 inatupatia alama nne za msingi za kila kanisa lenye afya. Isome kwa makini:
“Walidumu katika mafundisho ya mitume, na katika ushirika, na katika kumega mkate, na katika sala.”
Mambo ine. Si optional. Ndiyo uti wa mgongo wa maisha ya kanisa:
Mafundisho ya mitume — Neno linalofundishwa na kupokewa.
Ushirika (koinōnia) — maisha ya pamoja, si urafiki wa juu juu.
Kumega mkate — meza ya Bwana na chakula pamoja.
Sala — za pamoja na za binafsi, zinazodumu na zisizokoma.
Kisha ona kinachofuata: “walikuwa pamoja na walikuwa na vitu vyote kwa pamoja.” Waliuza mali na kuwapatia wenye mahitaji. Walikutana kila siku katika nyua za hekalu (nafasi ya public) na nyumbani kwao (nafasi ya privé). Walimsifu Mungu. Walipata kibali mbele ya watu wote. Na Bwana akaongeza kila siku kwa hesabu yao wale waliokuwa wakiokoka.
Hapo iko rythme: ibada ya public na ushirika wa nyumba. Hekalu na nyumba. Mukutano mkubwa na mukutano mdogo. Kanisa la nyumbani (oikos) linazaliwa hapa. Kila mouvement iliyojaa Roho hurudi kwenye rythme hii — na tutaiona tena katika missions zetu Afrika Mashariki na katika makanisa yetu mijini. Bwana hakutuita tu kwenye bâtiment siku ya Bwana. Alituita kwenye nyumba ya imani kila siku ya wiki.
SEHEMU YA 3 — MUJUE NENO: FOCUS YA MAFUNDISHO
Sasa tunasimama nyuma kidogo kutoka kwenye récit na kuangalia kile Matendo 2 inatufundisha juu ya Maandiko yenyewe.
1. Roho Huja Kupitia Neno na Ndani ya Neno
Pentekoste haikuzalisha Biblia mpya. Pentekoste ilizalisha watu ambao ghafla walijua Biblia waliyokuwa nayo tayari. Ona kwamba Petro — mvuvi ambaye hakufundishwa rasmi kama rabbi — ananukuu Yoeli, Zaburi 16, na Zaburi 110 katika mahubiri moja. Anapita kati ya Manabii na Zaburi kwa confiance. Roho aliyeshuka juu yake alimujaza Neno ambalo alikuwa akisikia kwa miaka mingi.
Somo kwetu liko wazi: usidharau kusoma Maandiko kila siku, hata wakati hujisiki kuwa umepakwa mafuta. Roho atatumia Neno ambalo tayari liko ndani yako wakati utakapofika. Biblia inayosomwa kwa privé inakuwa Biblia inayohubiriwa public.
2. Mahubiri ya Petro Yamejengwa Kabisa Juu ya Agano la Kale
Watu wengi wanafikiri Agano Jipya lilifanya Agano la Kale lisiwe la lazima. Mahubiri ya Petro yanathibitisha kinyume. Kila hoja kubwa katika Matendo 2:14–36 imejikita katika Maandiko ya Kiebrania. Mitume waliojaa Roho hawakuliacha Agano la Kale — walilifungua kwa ukamilifu zaidi na kutuonyesha namna yote inaelekeza kwa Kristo.
Unaposoma Agano lako la Kale, muulize Roho: “Nionyeshe Kristo katika kifungu hiki.” Biblia yote ni Biblia moja, na Yesu ndiye centre.
3. “Hiki Ndicho Kile” — Namna Roho Anavyosoma Biblia
Petro anatumia expression maalum katika Matendo 2:16: “Hiki ndicho kilichosemwa na nabii Yoeli.” Ile expression ndogo, “hiki ndicho kile,” ni namna ya kusoma Biblia kwa kuongozwa na Roho. Roho anaonyesha mahali ahadi zinatimizwa. Anaunganisha wakati wa sasa na Neno la Mungu lililosemwa zamani.
Jifundishe kusoma Maandiko namna hii. Unapokutana na wakati katika maisha yako, uliza: “Kuna ‘hiki ndicho kile’ hapa? Je, Mungu anatimizia kitu alichowahi kusema?”
SEHEMU YA 4 — MUTUMAINIE ROHO: FOCUS YA MAFUNDISHO
1. Roho Anazaa Kanisa Kupitia Neno, Si Kando ya Neno
Ona sequence: Roho anawajaza wanafunzi, wanafunzi wanazungumza, umati unasikia, Petro anahubiri, mioyo inachomwa, elfu tatu wanabatizwa. Kazi ya Roho haiwezi kutenganishwa na kazi ya Neno. Ni mkono wa kuume na wa kushoto wa Mungu yule yule. Wakristo wanapojaribu kuwa na Roho bila Neno, wanateleza kwenye machafuko. Wakristo wanapojaribu kuwa na Neno bila Roho, wanateleza kwenye ukavu. Matendo 2 hairuhusu kosa lolote kati ya hayo.
2. Kazi ya Kwanza ya Roho Ni Mission, Si Experience ya Mystique
Kitu cha kwanza Roho anafanya ni kusukuma wanafunzi kutoka chumba cha juu kwenda espace ya public. Hawaachi kukaa zaidi katika experience ya privé. Anawatuma. Roho anakujaza ili akutume. Tukimpokea Roho ili tumufurahie tu kwa privé, tumemuelewa vibaya.
3. Roho Ni kwa Watu wa Kawaida Katika Mahali pa Kawaida
Angalia nani walipokea Roho Pentekoste: wavuvi, watoza ushuru, wanawake wa Galilaya, ndugu za Yesu. Hakukuwa na celebrities. Hakukuwa na philosophes. Hakukuwa na wafalme. Roho alishuka juu ya watu wa kawaida, na kupitia wao dunia yote ilifikiwa.
Huhitaji pedigree ya ajabu ili ujazwe Roho. Unahitaji moyo ulio wazi na maisha ya utii. Roho ni kwa nyumba, kazini, sokoni, na kijijini.
Neno na Roho Katika Matendo 2 — Pembeni kwa Pembeni
Petro ananukuu Yoeli 2:28–32 kutafsiri Pentekoste (Matendo 2:16–21). | Roho anakuja na upepo, moto, na lugha — initiative ya Mungu, si ya binadamu (Matendo 2:1–4).
Petro ananukuu Zaburi 16 kutangaza ufufuo wa Kristo (Matendo 2:25–28). | Roho anachoma mioyo ya wasikilizaji — conviction inakuja kwa Roho (Matendo 2:37).
Petro ananukuu Zaburi 110:1 kutangaza kutawazwa kwa Kristo (Matendo 2:34–35). | Roho anatengeneza communauté ya maisha ya pamoja — ushirika unaumbwa na Roho (Matendo 2:42–47).
Kanisa la kwanza linajitoa kwa mafundisho ya mitume (Matendo 2:42). | Kanisa la kwanza linajitoa kwa sala na kumega mkate (Matendo 2:42).
SEHEMU YA 5 — KUMUUMBA KRISTO NDANI YA MUAMINI
Mwisho wa kila somo la School of Service si information. Ni transformation. Kristo kuumbwa ndani yako. Matendo 2 inamuumba Kristo ndani yetu kwa njia tatu:
Kristo anaumbwa ndani yetu wakati moto na Maandiko vinakutana katika maisha yetu. Usitenganishe kile Mungu ameunganisha. Tafuta Roho na tafuta Neno pamoja.
Kristo anaumbwa ndani yetu tunapotoka kuwa wasikilizaji na kuwa mashahidi. Pentekoste haikuwa baraka ya privé kwa wale waliokuwa chumba cha juu; ilikuwa kutumwa kwenda espace ya public. Kama umebarikiwa, umetumwa.
Kristo anaumbwa ndani yetu tunapoishi katika rythme ya kanisa la nyumbani. Neno, ushirika, mkate, sala — katika mikutano mikubwa na katika nyumba. Kanisa la kwanza lilifanya vyote viwili. Na sisi lazima tufanye hivyo.
SEHEMU YA 6 — MASWALI YA MAJADILIANO
Haya ndiyo maswali tutakayopitia pamoja darasani. Uje umejiandaa kujibu, na uje umejiandaa kusikiliza.
Roho alitolewa siku ambayo Mungu alikuwa ameiweka alama karne nyingi mbele. Ni wapi katika maisha yako mwenyewe unaona Mungu alikuwa tayari akikukuandaa, zamani kabla hujaelewa?
Petro alihubiri Kristo kutoka Agano la Kale. Unalijua Agano la Kale kwa kiwango gani? Ungeanzia wapi kukua wiki hii?
Roho anazungumza katika kila lugha. Ni “lugha” gani — culture, profession, génération, quartier — Mungu anakutuma uizungumzie injili?
Kanisa la kwanza lilikuwa na alama nne: mafundisho, ushirika, kumega mkate, na sala. Ni ipi kati ya nne iliyo zaifu zaidi katika maisha yako sasa? Hatua moja ya kuiimarisha ni ipi?
Elfu tatu waliokoka siku moja. Je, kweli unatarajia Mungu kufanya kazi kwa nguvu kubwa katika wakati wetu? Kwa nini au kwa nini hapana?
SEHEMU YA 7 — KAZI YA WIKI
Kabla ya darasa linalofuata, chukua wakati kwa mambo haya:
Soma Matendo 3 kujiandaa kwa Somo la Tatu.
Kariri Matendo 2:42.
Soma kifungu kimoja cha Agano la Kale kinachonukuliwa katika Matendo 2 — Yoeli 2:28–32, Zaburi 16, au Zaburi 110 — na umuombe Roho akuonyeshe Kristo ndani yake.
Fungua nyumba yako kwa ushirika angalau mara moja wiki hii — alika ndugu, dada, jirani, au familia. Fanya pratique ya pattern ya nyumba ya Matendo 2:42–47.
Tambua mutu mmoja aliye “mbali” — mutu ambaye kwa kawaida hungezungumza naye juu ya Kristo — na umuombee kila siku wiki hii.
SALA YA KUFUNGA
SALA YA KUSALI KWA SAUTI WIKI HII
Bwana Yesu, Kristo uliyetukuzwa, ulimimina Roho wako ili nikujue. Washa Neno kama moto ndani yangu. Usiniache niwe na moto bila Maandiko, wala usiniache niwe na Maandiko bila moto.
Tengeneza ndani yangu moyo wa Petro — wenye ujasiri, uliorudishwa, uliojaa Neno lako, tayari kusimama na kuinua sauti yangu. Okoa elfu tatu unaowaita katika génération yetu, na unitume nyumbani kwangu, kazini kwangu, kwa familia yangu, na quartier yangu pamoja na injili ya ufufuo wako.
Ifanye nyumba yangu kuwa nyumba ambamo Neno linafundishwa, mkate unamegwa, ushirika ni wa kweli, na sala ni ya kudumu. Roho mwenye utukufu, ushuke juu yangu tena. Katika Jina la Yesu, amina.
SOMO LINALOFUATA
Somo la Tatu — Matendo 3