Bonyeza hapa upate orodha ya masomo.
Masomo kwa WhatsApp
Kama kusoma kwenye internet ya kawaida ni gharama kubwa, masomo ya Shule ya Huduma ya KGM yanapangwa kupatikana ndani ya WhatsApp, mahali mitandao mingi ya Afrika Mashariki na Maziwa Makuu hutoa vifurushi vya bei nafuu.
Kupokea masomo kwa WhatsApp kumefunguliwa. Mwendeshaji wa KGM anajibu ujumbe wako mkono kwa mkono. Tovuti hii pia ni maktaba kamili — kila somo lililochapishwa liko hapa kusoma ao kupakua.
Namba ya WhatsApp ya KGM School ni: +1 581 580 5772. Ihifadhi kwenye simu yako, kisha bonyeza kiungo cha kijani hapo juu kuanza mazungumzo.
WhatsApp inakusudiwa kuwa njia kuu ya kutoa masomo kwa kutumia data kidogo. Tovuti hii ni maktaba rasmi, lakini WhatsApp imetengenezwa kwa wachungaji wanaolipia data kwa megabyte.
Namna itakavyofanya kazi
Tuma amri fupi kwa WhatsApp ya KGM School. Kila amri inaanza na msimbo wa kozi ili kozi inayofaa ijibu.
Kwa ujumla
- Tuma MENU kuanza.
- Tuma HELP kufikia mtu wa KGM.
- Tuma STOP kusimamisha ujumbe.
Yako tayari sasa:
- Tuma KGM EN 01 kupata Somo la 1 la KGM School kwa Kiingereza.
- Tuma KGM FR 01 kupata Somo la 1 la KGM School kwa Kifaransa.
- Tuma PSOS EN 01 kupata Somo la 1 la Potter’s School kuhusu Matendo ya Mitume kwa Kiingereza.
- KGM RW 01 — Kinyarwanda
- KGM RN 01 — Kirundi
- KGM LG 01 — Luganda
- KGM SWTZ 01 — Kiswahili Tanzania
- KGM SWCD 01 — Kiswahili Kongo Mashariki
Yatakuja karibuni:
TSOS SWTZ 01— Shule ya Tanzania kwa Kiswahili
Itakugharimu nini?
- Ujumbe wa maandishi ndani ya WhatsApp mara nyingi ndiyo njia ya bei nafuu. Mitandao mingi huweka WhatsApp katika vifurushi maalum.
- Viungo vya tovuti hufunguka kwenye browser na hutumia data ya kawaida ya simu.
- PDF na sauti ziombwe tu kama una kifurushi cha WhatsApp kinachoruhusu kupakua mafaili, ao kama una data ya kutosha.
Siri na heshima
- Hatutakutumia masomo ambayo hujaomba. Utapokea ujumbe baada ya kutuandikia kwanza.
- Hatutatumia ujumbe wa matangazo. Shule hii ni huduma, si kampeni.
- Unaweza kutuma STOP wakati wowote.
- Tuma HELP kuunganishwa na mtu wa KGM.
- Namba yako ya simu haitachapishwa mahali popote kwenye tovuti.
Bonyeza hapa upate orodha ya masomo.